WHO yataka nyongeza ya ushuru wa ulevi kupunguza vifo
6 Desemba 2023Matangazo
Baada ya kufanya tafiti za viwango vya ushuru, WHO imesema kuwa kiwango cha wastani cha ushuru kimataifa kwa "bidhaa zisizo bora kiafya" kilikuwa cha chini mno, huku ikisisitiza kuwa bidhaa kama vile mvinyo hazitozwi kabisa ushuru katika baadhi ya nchi za Ulaya.
Soma zaidi: WHO kutanua utolewaji chanjo ya Malaria kwa watoto Afrika
Kulingana na WHO, watu milioni 2.6 hufariki kila mwaka kutokana na kunywa pombe huku watu milioni 8 wakifariki pia kwa mwaka kutokana na ulaji usiofaa.
Shirika hilo limesema kuongeza ushuru kutasaidia kupunguza matumizi ya bidhaa hizo na kutoa motisha kwa makampuni kutengeneza bidhaa zenye ubora kwa afya ya binaadamu.