1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WHO yasema dawa ya kikohozi ya J&J haipatikani tena Afrika

Sylvia Mwehozi
23 Aprili 2024

Shirika la afya ulimwenguni, WHO, limesema kuwa dawa ya majimaji ya kikohozi kwa watoto iliyogunduliwa kuwa na viambata vya sumu haipatikani tena katika nchi za Kiafrika ambako ilikuwa inauzwa.

https://p.dw.com/p/4f5Tu
WHO yasema dawa ya kikohozi inayodaiwa kuwa na viambata vya sumu haipatikani tena Afrika
WHO yasema dawa ya kikohozi inayodaiwa kuwa na viambata vya sumu haipatikani tena AfrikaPicha: Lev Dolgachov/Zoonar/picture alliance

Mapema mwezi huu, Nigeria ilipiga marufuku dawa ya kikohozi na mzio kwa watoto baada ya vipimo kugundua kwamba ilikuwa na viwango vya sumu.

Nchi nyingine tano za Afrika pia zilipiga marufuku dawa hiyo ambazo ni Kenya, Rwanda, Tanzania, Zimbabwe na Afrika Kusini.

Dawa hiyo ya kikohozi imetengenezwa na kampuni ya Johnson & Johnson nchini Afrika Kusini. Hakuna mtoto ambaye ameripotiwa kudhulika na dawa hiyo.

Viambata vya sumu vinavyotajwa vinaweza kusababisha kushindwa kufanya kazi kwa figo na vinahusishwa na vifo vya zaidi ya watoto 300 nchini Cameroon, Gambia, Indonesia na Uzbekistan tangu 2022.