1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WHO: Ulaya inakabiliwa na maamuzi makubwa kuhusu afya

10 Machi 2022

Shirika la Afya Ulimwenguni, WHO limetoa mwito kwa mataifa ya Ulaya kuzingatia zaidi suala la afya kuliko ilivyokuwa kabla ya janga la virusi vya corona.

https://p.dw.com/p/48JNj
Themenbild-novavax Tot Impfstoff.
Picha: Frank Hoermann/SvenSimon/picture alliance

Ofisi ya WHO barani Ulaya, imesema katika uzinduzi mpya wa Ripoti ya Afya ya Ulaya ya mwaka 2021 kwamba nchi zinakabiliwa na changamoto katika kutatua usawa na kufikia malengo yanayohusu afya yaliyojumuishwa katika Malengo ya Maendeleo Endelevu ya 2030 ya Umoja Ulaya. Mkurugenzi wa WHO barani Ulaya, Hans Kluge, amesema miaka miwili tangu kuanza kwa janga la virusi vya corona, sasa kuna muelekeo wa wazi kwa serikali kuamua kuipa sekta ya afya kipaumbele cha juu zaidi kuliko hapo awali na kuzingatia masuala ambayo yamepuuzwa kwa muda mrefu kama vile afya ya akili na ustawi wa wananchi walio katika hatari. Lakini shirika hilo pia limesema sasa kuna nafasi ya kuchukua maamuzi muhimu ambayo yataunda mustakabali wa Ulaya. Ripoti ya Afya ya Ulaya huchapishwa kila baada ya miaka mitatu na shirika la WHO barani Ulaya. Ripoti ya mwaka huu ina zaidi ya kurasa 300, ambazo zinaangalia maendeleo ya nchi 53 barani Ulaya.