WHO yaridhia chanjo mpya ya malaria kwa watoto
3 Oktoba 2023Matangazo
Takriban watoto nusu milioni katika kanda ya Afrika hufa kila mwaka kutokana na ugonjwa huo unaosababishwa na vimelea vinavyoenezwa na mbu.Mkuu wa Shirika la Afya Duniani Tedros Adhanom Ghebreyesus amenukuliwa akiseama "Kama mtafiti wa malaria, nilikuwa na ndoto ya siku ambayo tutakuwa na chanjo salama na yenye ufanisi dhidi ya malaria. Sasa tuna mbili."Chanjo mpya aina ya R21/Matrix-M, iliyoendelezwa na Chuo Kikuu cha Oxford cha Uingereza na kutengenezwa na taasisi ya Serum ya India, tayari imeidhinishwa kutumika nchini Burkina Faso, Ghana na Nigeria.