WHO: Afrika yachangia kuongezeka kwa visa vya surua duniani
30 Novemba 2018Shirika ya Afya Duniani WHO limesema hali ya wasiwasi wa kugunduliwa upya kwa visa vya surua unakaribia kuwa tukio linaloihusu dunia kwa ujumla,lakini sababu zinatofautiana miongoni mwa maeneo. Katika bara la Ulaya, wataalamu wamesema tatizo hilo linatokana na habari mbaya kuhusu chanjo ya surua ambayo imethibitishwa kuwa bora na salama.
Mkuu wa masuala ya chanjo katika WHO Martin Friede amesema kashafa inayotolewa na baadhi ya wanaojiita wataalamu kuhusu chanjo hiyo bila kuwa na ushahidi, wameathiri maamuzi ya wazazi. Amekosoa madai yanayosambazwa kwenye mitandao ya kijamii kwamba chanjo hiyo inasababisha tawahudi. Lakini visa vya surua vimeongzeka katika Amerika ya Kusini kutokana na kudhoofika kwa mifumo ya afya nchini Venzuela.
Mataifa mengi yakiwemo Ujerumani, Urusi na Venezuela wamepokonywa cheti cha kukabili surua katika muda wa mwaka mmoja uliopita. Taifa hupoteza cheti hicho wakati virusi vya ugonjwa huo vinasambaa kwa zaidi ya miezi kumi na miwili mfululizo kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani WHO. Shirika hilo hata hivyo limesisitiza kuwa mapambano dhidi ya surua duniani yameonyesha matokeo mazuri katika karne hii.
Mwaka 2000 kuliwepo na visa elfu 8850 vilivyoripotiwa duniani, ikilinganishwa na visa elfu 173 mwaka uliopita. Kulingana na miongozo ya WHO, kukabili surua kunahitaji asilimia 90 ya chajo katika awamu ya kwanza. Chanjo hiyo imekuwa ikitolewa kwa asilimia 85 kwa miaka mingi, lakini kiwango hicho ni cha chini katika maeneo ya Afrika, ambayo yalikuwa na asilimia 70 mwaka 2017.
Surua ni ugonjwa unaomabukizwaambao unweza kusababisha kuharisha vibaya, homa ya mapafu na kupoteza uwezo wa kuona na wakati mwingine kusababisha vifo. Mwaka uliopita mambukizi elfu 190 na vifo elfu 110 vilinakiliwa kote duniani, lakini idara ya afya ya Umoja wa Mataifa inakadiria kuwa idadi kamili ya visa hivyo ni watu milioni 6.7. Wagonjwa wengi waliofariki dunia walikuwa watoto.
Mwandishi: Sophia Chinyezi/DPAE/AFPE
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman