1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WHO : Afrika inaweza kutokomeza Mpox ndani ya miezi sita

Angela Mdungu
31 Agosti 2024

Mkuu wa Shirika la Afya Ulimwenguni , Tedros Adhanom Ghebreyesus, amesema anaamini kuwa maambukizi ya virusi vya homa ya nyani, yanaweza kutokomezwa ndani ya miezi sita ijayo.

https://p.dw.com/p/4k82V
Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema anaamini kuwa maambukizi ya virusi vya Mpox, yanaweza kutokomezwa ndani ya miezi sita ijayo
Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema anaamini kuwa maambukizi ya virusi vya Mpox, yanaweza kutokomezwa ndani ya miezi sita ijayoPicha: Fabrice Coffrini/AFP/Getty Images

Ghebreyesus amesema licha ya kuwa maambukizi ya ugonjwa huo yamekuwa yakiongezeka kwa kasi, vifo vinavyotokana na maradhi hayo ni vichache. Licha ya kauli yake, hadi sasa bara la Afrika lenye maambukizi mengi zaidi limepokea kiasi kidogo cha chanjo dhidi ya mpox.

Hata hivyo Ghebreyesus amesema awamu ya kwanza ya chanjo kutoka kwa shirika lake zitawasili nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo ndani ya siku chache. Taifa hilo ndilo lenye idadi kubwa ya maambukizi. Hadi sasa watu 18,000 wameripotiwa kuwa na maambukizi ya homa ya nyani nchini humo na wengine 629 wameshafariki dunia.

Mataifa mengine yaliyoripoti kuwa na wagonjwa wenye maambukizi ya aina mpya ya virusi hivyo ni pamoja na Burundi, Rwanda, Kenya, Uganda, Sweden na Thailand.