WELLINGTON:Matokeo ya mwanzo yaashiria ushindi wa chama cha Labour
17 Septemba 2005Matangazo
Matokeo ya mwanzo ya uchaguzi nchini New Zealand yameashiria kuwa chama cha Labour cha Waziri Mkuu Helen Clark kimenyakua viti hamsini kikifuatiwa kwa karibu na chama cha upinzani cha National Party kilichopata viti 49.
Chama cha National Party kinaongozwa na Don Brash.
Wachunguzi wanasema huenda wapinzani wakaungana na vyama vidogo kama vile New Zealand First Party, chama cha Kijani na New Maori Party.
Clark anagombea kipindi cha tatu cha miaka mitano madarakani baada ya kuimarisha uchumi wa nchi hiyo katika kipindi chake cha utawala kilichopita.
Kwa upande wake, Brash ambaye ni gavana wa zamani wa benki kuu ya nchi hiyo, aliahidi kupunguza ushuru.