1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WEIMAR: Miaka 60 ya kambi ya mateso yaadhimishwa.

11 Aprili 2005
https://p.dw.com/p/CFOA

Wahanga 150 kutoka Mittelbau Dora wamejumuika na wanasiasa wa Ujerumani na wageni kutoka sehemu mbali mbali za dunia huko Ujerumani Mashariki kuadhimisha miaka 60 tangu kambi ya mateso ya mafashisti wa kinazi ya Buchenwald ilipokombolewa.

Wageni wa kimataifa wameadhimisha siku hii kwa kuweka mashada ya mauwa vilevile kuhudhuria tamasha ya filamu na michezo ya kuigiza kuwakumbuka wahanga kambi ya Buchenwald.

Wanajeshi wa Marekani waliokuwa wa mwanzo miongoni mwa wanajeshi shirika kuingia katika kambi hiyo waliwaokoa baadhi ya wahanga wa Buchenwald siku kama ya leo tarehe 11.04 1945.

Kansela Gerhard Schröeder akihutubia katika kumbukumbu hiyo alisema kuwa Ujerumani ya leo ni nyingine yenye maongozi ya kidemokrasia na itakua macho daima kuhakikisha visa vya unyonge,ubaguzi na chuki havipati nafasi ya kuchipuka.