1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUjerumani

Uingereza yaiomba Ujerumani kuipatia Ukraine makombora

26 Aprili 2024

Aliyewahi kuwa Waziri wa Ulinzi wa Uingereza Ben Wallace amemtolea wito Kansela wa Ujerumani Olf Scholz kukubali kuipatia Ukraine makombora ya masafa marefu ya Taurus.

https://p.dw.com/p/4fCSt
Kombora la Taurus
Ujerumani imekuwa na wasiwasi juu ya kusambaa kwa vita kati ya Urusi na Ukraine ikiwa itaipatia Ukraine makombora ya TaurusPicha: Sven Eckelkamp/IMAGO

Ujerumani imekuwa ikipinga hatua hiyo ya kuipatia makombora ya Taurus Ukraine, licha ya miito ya kila mara kutoka Kiev.

Wallace amesema ingawa anatambua sababu za Scholz kuwa na wasiwasi wa uwezekano wa kusambaa kwa mzozo, lakini wasiwasi huo hauna msingi na kuongeza kuwa wameshuhudia kwenye mzozo huo Urusi ikivuka mipaka yake.

Amesema, wanaweza kupatia Ukraine makombora hayo na kuwapa maelekezo ya mahala wanapotaka yatumike, akiamini kwamba Ukraine itakuwa tayari kuheshimu maagizo hayo.

Wallace aidha, amekosoa juu ya mawasiliano duni ambayo amesema yanadhoofisha hata zaidi msaada wa Ujerumani nchini Ukraine.