1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaLibya

Waziri wa zamani achiliwa huru na vikosi vya serikali

16 Julai 2023

Mamlaka ya usalama katika mji mkuu wa Libya Tripoli imemuachilia huru waziri wa fedha wa zamani Faraj Bumatari baada ya kuwekwa kizuizini na kusababisha kabila la Al-Zawi kufunga mitambo muhimu ya kuzalisha mafuta.

https://p.dw.com/p/4Txuo
Oil Terminal Az Zuwaytina
Picha: Maurizio Gambarini/dpa/picture alliance

Mamlaka ya usalama katika mji mkuu wa Libya Tripoli imemuachilia huru waziri wa fedha wa zamani Faraj Bumatari baada ya kuwekwa kizuizini na kusababisha kabila la Al-Zawi kufunga  mitambo muhimu ya kuzalisha mafuta.

Kulingana na vyombo vya habari vya ndani, Bumatari alikamatwa mapema wiki hii na shirika la usalama wa taifa lenye makao yake mjini Tripoli, ambalo linashirikiana na serikali ya Waziri Mkuu Abdul Hamid Dbeibah baada ya ombi lake la kutaka kuchukua nafasi ya Sadiq al-Kabir  kama gavana wa Benki Kuu ya Libya.

Soma pia: Libya magharibi, yatishia kuzuia usafirishaji mafuta

Ili kulazimisha kuachiliwa kabila analotoka Bumatari, la Al-Zawi lilifunga maeneo muhimu ya kuzalisha mafuta ya Elfeel, Sharara na maeneo mengine 108. Mtambo wa Sharara ni moja ya mitambo mikubwa zaidi nchini humo na una uwezo wa kuzalisha mapipa 300,000  ya mafuta kwa siku.