1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Waziri wa usafirishaji Singapore kizimbani kwa ufisadi

24 Septemba 2024

Waziri wa zamani wa usafirishaji wa Singapore anapandishwa mahakamani kwenye kesi ya kwanza ya ufisadi wa kisiasa baada ya zaidi ya miongo minne iliyoitikisa nchi hiyo inayotajwa kuwa na rikodi nzuri ya uwajibikaji.

https://p.dw.com/p/4kzye
Waziri Mkuu wa Singapore, Lawrence Wong.
Waziri Mkuu wa Singapore, Lawrence Wong.Picha: Singapore Press/AP Photo/picture alliance

S. Iswaran alijiuzulu mnamo mwezi Januari baada ya kukabiliwa na mashitaka kadhaa kama sehemu ya uchunguzi wa ufisadi, ikiwemo kupokea zawadi zenye thamani ya dola 300,000 za Kimarekani kutoka kwa wafanyabiashara.

Kesi yake inatajwa na waangalizi kama mojawapo ya hatua muhimu sana kwenye historia ya nchi hiyo na iliyoathiri sana heshima ya chama tawala cha PAP kuelekea uchaguzi mkuu wa mwakani.

Soma zaidi: Maoni: Afrika Mashariki bado yanuka ufisadi

Waziri Mkuu wa Singapore, Lawrence Wong, amesema msimamo wa chama chake dhidi ya ufisadi hautikisiki. Mara ya mwisho kwa mtumishi wa ngazi za juu wa umma kushitakiwa kwa ufisadi ilikuwa ni mwaka 1975, pale Wee Toon Boon, alipotuhumiwa kwa rushwa ya dola 600,000 za Kimarekani.