1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri wa ulinzi wa Uingereza aizuru Iraq

19 Oktoba 2008
https://p.dw.com/p/Fcvk

Baghdad:

Waziri mpya wa ulinzi wa Uingereza John Hutton amefanya ziara yake ya kwanza nchini Irak leo na amekua na mazungumzo na Waziri mkuu wa nchi hiyo Nuri al-Maliki mjini Baghdad. Bw Hutton aliyekua awali Waziri wa biashara, amechukua wadhifa huo mpya baada ya mabadiliko ya baraza la mawaziri yaliofanywa na Waziri mkuu Gordon Brown tarehe 3 mwezi huu. Uingereza ina jumla ya wanajeshi 4.000 nchini Irak , sehemu kubwa wakiwa katika kambi moja ya jeshi la anga, nje ya mji wa kusini wa Basra. Uingereza sawa na Marekani zinajadiliana na Irak kuhusu makubaliano ya pamoja, yatakayo yaruhusu majeshi yao kubakia Irak, baada ya kumalizika muda ulioidhinishwa na Baraza la usalama la Umoja wa mataifa, mwishoni mwa mwaka huu.