Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani ziarani kanda ya Balkan
26 Agosti 2010Matangazo
Mada kuu ya majadiliano yake katika mji mkuu wa Serbia Belgrade,ni mgogoro unaohusika na suala la kuutambua uhuru wa Kosovo.
Majadiliano yanayohusika na uanachama wa Serbia katika Umoja wa Ulaya, hayakufanikiwa mpaka hivi sasa kwa sababu ya nchi hiyo kukataa kutambua uhuru wa Bosnia. Hii leo mjini Belgrade, waziri Westerwelle atakutana na Rais Boris Tadic na maafisa wengine wa Serbia.
Westerwelle alianzia ziara yake nchini Croatia na aliarifu kuwa nchi hiyo inakaribia kukamilisha utaratibu wa kuingia katika Umoja wa Ulaya.
Mhariri: P.Martin/ZPR