Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Maas, ziarani Afrika
3 Septemba 2019Matangazo
Maas anakuwa mwanadiplomasia wa kwanza wa ngazi ya juu wa Ulaya kukutana na uongozi mpya wa nchi hiyo. Maas amesema kwamba Sudan ipo katika mabadiliko ya kihistoria na kwamba wanataka kuunga mkono uongozi mpya katika jukumu zito la kuifungua milango ya nchi, kufanya mageuzi na maandalizi ya uchaguzi wa kidemokrasia. Aidha ameongeza kwamba huu ni wakati wa Sudan kutumia nafasi hiyo, kupokea uungwaji mkono kutoka Jumuiya za kimataifa. Maas ataitembelea pia Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Jumanne jioni, ambapo miongoni mwa mambo mengine, atapata taarifa za ujumbe wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa MONUSCO pamoja na mapambano dhidi ya ugonjwa wa mripuko wa ebola. Maas ataitembelea Kivu ya Kaskazini ambayo imeathiriwa vibaya na ugonjwa huo.