Ujerumani kuisaidia Ukraine kukabiliana na vita vya Urusi
21 Juni 2023Baerbock ameahidi kwamba Ujerumani itatowa msaada kwa Ukraine katika kipindi cha mwaka huu, ambazo zitatumika kusimamia kwa mfano ununuzi wa majenereta chakula na mahema.
Fedha sio hatua ya kutosha kuisaidia Ukraine
Hata hivyo waziri huyo wa Ujerumani ameongeza kusema kwamba fedha sio hatua ya kutosha kuisadia Ukraine na kwamba Ujerumani itasaidia nchi hiyo katika kuwekeza kwenye nishati mbadala na nishati ya uhakika.
Blinken atangaza msaada wa Marekani wa dola bilioni 1.3
Katika mkutano huo wa mjini London, awali pia waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken alitangaza msaada wa dola bilioni 1.3 utakaotolewa na nchi yake kwa ajili ya kuisadia ukraine ambapo milioni 520 zimekusudiwa kusaidia katika shughuli za ukarabati wa gridi ya nishati ya Ukraine.Uingereza inayoongoza mkutano huo kwa pamoja na Ukraine, imesema makampuni chungu nzima yametangaza kuwa tayari kuisadia Ukraine