1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Annalena Baerbock aanza ziara katika eneo la Ghuba

15 Mei 2023

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani, Annalena Baerbock, anatarajiwa kufanya mazungumzo na mwenzake wa Saudi Arabia, Faisal bin Farhan, katika mji wa bandari wa Jeddah

https://p.dw.com/p/4RMLe
Schweden | informelles Treffen der EU-Außenminister in Stockholm
Picha: Kira Hofmann/photothek/picture alliance

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ameeleza kuwa mazungumzo hayo yanatarajiwa kujikita kando na mambo mengine, juu ya mzozo nchini Sudan na Yemen ambayo ni jirani wa Saudi Arabia kwa upande wa kusini.

Bearbock pia anatarajiwa kufanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Yemen, Ahmed bin Mubarak, mjini Jeddah, pamoja na mratibu wa Umoja wa Mataifa kwa Yemen, David Gressly.

Miongoni mwa masuala ya sera za kigeni katika ajenda ya mkutano huo ni kuhalalisha uhusiano kati ya Saudi Arabia na Iran, na kurudi kwa Syria ndani ya Jumuiya ya Nchi za Kiarabu kufuatia kusimamishwa kwake Novemba 2011.