1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa ziarani Iraq

31 Mei 2008

-

https://p.dw.com/p/EAGB

Waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa Bernerd Kouchner amefanya ziara ya ghafla kusini mashariki mwa Iraq katika mji wa Nasiriya akitokea Jordan ambako amesaini makubaliano ya kuisaidia nchi hiyo kuanzisha mpango wa nishati ya nuklia kwa ajili ya matumizi ya amani.

Kouchner amekutana na makamu wa rais Abdel Abdul Mahdi pamoja na gavana wa jimbo hilo la Iraq Aziz Kadhim Alwan hii leo.

Waziri huyo wa mambo ya nje wa Ufaransa amesema ziara yake nchini Iraq inatoa ujumbe mahsusi wa amani na ushirikiano pamoja na nafasi ya kujadiliana juu ya mchango wowote wa baadae wa Ufarasa katika kuijenga upya Iraq.Aidha amesema watoto wanne wakiiraqi ambao wanahitaji kufanyiwa upasuaji wa moyo watasafirishwa Ufaransa kufanyiwa upasuaji huo.