1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Blinken aanza ziara nyingine ya Mashariki ya Kati

5 Februari 2024

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken anaelekea Mashariki ya kati leo Jumatatu katika ziara nyingine ya kujaribu kutafuta makubaliano mapya ya kusitisha vita kati ya Israel na kundi la Hamas.

https://p.dw.com/p/4c2o3
Antony Blinken
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony BlinkenPicha: Mark Schiefelbein/AP Photo/picture alliance

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken anaelekea Mashariki ya kati leo Jumatatu katika ziara nyingine ya kujaribu kutafuta makubaliano mapya ya kusitisha vita kati ya Israel na kundi la Hamas.

Vita bado vinaendelea Kusini mwa Gaza. Kabla ya ziara hiyo mwanadiplomasia huyo wa ngazi za juu wa Marekani amesisitiza haja ya kushughulikiwa haraka suala la mahitaji ya kibinadamu katika Gaza, baada ya mashirika ya msaada kutahadharisha mara kadhaa kuhusu hali mbaya kwenye eneo hilo lililozingirwa katika kipindi cha takriban miezi mitano ya vita.

Katika ziara yake hiyo ya tano katika Mashariki ya Kati, Blinken anatarajiwa pia kwenda Saudi Arabia, Israel, Misri na Qatar.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW