Matangazo
Ziara yake inafanyika katika wakati utawala wa rais mpya wa Iran Ibrahim Raisi unatafuta kuimarisha uhusiano zaidi na mataifa yanayoendelea. Lakini taifa kama Tanzania linanufaika vipi na mahusiano na Iran? Hilo ni miongoni mwa maswali ambayo Rashid Chilumba amemuuliza Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje ya Bunge la Tanzania, Vita Kawawa akiwa jijini Dar es Salaam.