Waziri wa Mambo ya Ndani wa Somalia auwawa
11 Juni 2011Matangazo
Ionekanavyo, shambulizi hilo lilifanywa na mpwa wake wa kike. Hiyo ni kwa mujibu wa afisa wa ngazi za juu wa Somalia, Adan Mohamed. Vyanzo vingine vya usalama vinasema mwanamke huyo aliishi katika nyumba ya waziri huyo tangu siku tatu zilizopita.
Kiongozi wa kundi la waasi la al-Shebab ametangaza kuwa wao ndio waliohusika na shambulio lililomuuwa waziri huyo.
Mwandishi: Sudi Mnette
Mhariri: Prema Martin