Waziri wa mambo ya kigeni wa Urusi yuko ziarani Cairo
16 Septemba 2024Mwanadiplomasia huyo wa ngazi za juu wa Urusi akizungumza baada ya mazungumzo yake na mwenzake wa Misri Badr Abdelatty,mjini Cairo, amesema Urusi inakaribisha juhudi za kushinikiza kufikiwa makubaliano ya kusitisha vita vilivyodumu miezi 11.
Ameishutumu Marekani akisema nchi hiyo haitaki kupitisha maamuzi yoyote yanayoungwa mkono na kila mtu,kumaliza vita Gaza.
Soma pia: Israel na Misri zaruhusu misaada ya kibinaadamu kupelekwa Gaza
"Na kama maazimio ya baraza la usalama la Umoja wa Mataifa,kuhusu vita kati ya Israel na Hamas katika Gaza yalivyopitishwa bila ya mwafaka,hivyo ndivyo yalivyobakia hadi hivi sasa. Hakuna ahadi za Marekani zilizotimizwa. Lakini haimaanishi kwamba tunapaswa kuziachia hapo juhudi zetu," alsiema Lavrov.
Kundi la Hamas linataka yawepo makubaliano ya kudumu ya usitishaji vita na kuondoka kikamilifu kwa vikosi vya Israel kutoka Gaza kama sehemu ya makubaliano ya kuwaachia huru mateka raia wa Israel inayowashikilia.