1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Ujerumani kuizuru China

12 Aprili 2023

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Annalena Baerbock anatarajiwa kusafiri kuelekea China baadaye wiki hii katika ziara yake ya kwanza nchini humo huku lengo likitarajiwa kuwa Ukraine.

https://p.dw.com/p/4PxzN
Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Ujerumani, Annalena Baerbock
Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Ujerumani, Annalena Baerbock Picha: Geert Vanden Wijngaert/AP/picture alliance

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Wang Wenbin amewaambia wanahabari mjini Beijing kwamba Baerbock atafanya awamu ya sita ya mazungumzo ya kimkakati kati ya mataifa hayo mawili na waziri mpya wa mambo ya nje Qin Gang, wakati wa ziara hiyo itakayoanza siku ya Alhamisi hadi Jumamosi.

Pamoja na uhusiano kati ya nchi hiyo mbili na uhusiano na Umoja wa Ulaya, mawaziri hao wawili wanatarajiwa kuangazia kuhusu matatizo ya kimataifa na kikanda.

Baerbock anatarajiwa pakubwa kuangazia uvamizi kamili wa Urusi nchini Ukraine ambao China bado haijalaani.