1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri wa Kongo asema nchi hiyo haishughulikiwi kimsaada

22 Mei 2023

Waziri wa masuala ya mshikamano wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo Modeste Mtinga amesema akiwa mjini Geneva kwamba, mgogoro wa nchi yake umepuuzwa na Jumuiya ya Kimataifa ikilinganishwa na mgogoro wa Ukraine.

https://p.dw.com/p/4Rfz3
Genf Spanisches Zimmer der Vereinten Nationen
Picha: Jean-Marc Ferre/UN Photo

Kongo imesema kwamba mwito wa kutolewa msaada wa kibinadamu uliotolewa na Umoja wa Mataifa, umefadhiliwa kwa asilimia 20 tu na Jumuiya ya Kimataifa wakati nguvu kubwa ikielekezwa katika kuisadia Ukraine.

Ameongeza kusema, kwamba nchi  nyingi za Ulaya na kwengineko zimetowa msaada mkubwa kwa Ukraine  kuwasaidia watu walioathirika linapohusika suala la msaada wa kibinadamu.

Bruno Lemarquis ambaye ni mratibu wa msaada wa kibinadamu nchini Kongo amesema katika dola bilioni 2.25 zinazohitajika mwaka huu kuisadia Kongo,ni asilimia 20 zilizotolewa.