1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri wa elimu Ujerumani ashtushwa na kifo cha mwalimu

11 Januari 2023

Waziri wa elimu wa Ujerumani Bettina Stark-Watzinger leo ameelezea kushtushwa na kifo cha mwalimu aliyeuwawa kwa kuchomwa kisu na mwanafunzi jana Jumanne.

https://p.dw.com/p/4M260
Deutschland Bundesbildungsministerin Bettina Stark-Watzinger
Picha: Chris Emil Janssen/IMAGO

Waziri huyo ameuambia wavuti wa habari wa t-online kwamba kifo hicho kimewashangaza na sharti wafanye kila linalowezekana kuwalinda vyema zaidi walimu kutokana na machafuko.

Pia amesema haikubaliki kwamba walimu wanatukanwa mara kwa mara, kutishwa na kushambuliwa.

Wachunguzi wanasema mwanafunzi mwenye umri wa miaka 17 anayeshukiwa kwa mauaji hayo alimtembelea mwalimu huyo mwenye umri wa miaka 55 aliyekuwa peke yake katika chuo cha ufundi cha mji wa Ibberbüren magharibi mwa Ujerumani jana mchana.

Baadaye aliwapigia simu polisi na kuwaruhusu wamkamate bila upinzani wowote.

Sababu ya kumshambulia mwalimu wake haijafahamika.

Msemaji wa polisi amesema mwili utafanyiwa uchunguzi leo na mshukiwa atapandishwa kizimbani leo.