Waziri Steinmeier akamilisha ziara ya Asia ya Kusini-Mashariki
1 Machi 2008Matangazo
HANOI:
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Frank Walter Steinmeier amekamilisha ziara yake ya Asia ya Kusini-Mashariki kwa kutembelea jiji kuu la biashara Ho-Chi-Minh kusini mwa Vietnam.Steinmeier vile vile ametia saini makubaliano ya kuanzishwa majadiliano kuhusu utawala wa kisheria,kama alivyofanya na serikali ya China miaka michache iliyopita.Vile vile kwa msaada mkubwa wa jimbo la Hessen la Ujerumani,kutajengwa chuo kikuu cha Vietnam na Ujerumani katika jiji la Ho Chi Minh.Inatarajiwa kuwa chuo kikuu hicho kitakuwa tayari kupokea wanafunzi katika mwaka 2009.Vietnam ni kituo cha mwisho cha ziara ya siku sita iliyofanywa na waziri Steinmeier katika Asia ya Kusini-Mashariki.Ziara hiyo ilimpeleka Indonesia na Singapore pia.