1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Waziri mkuu wa zamani wa Pakistan arejea nyumbani

13 Mei 2023

Waziri mkuu wa zamani wa Pakistan, Imran Khan amerejea nyumbani leo baada ya kuachiwa kwa dhamana, kufuatia siku kadhaa za mvutano wa kisheria na ghasia za nchi nzima kupinga kukamatwa kwake kwa tuhuma za ufisadi.

https://p.dw.com/p/4RIiY
Pakistanischer Ex-Premier Khan vorübergehend freigelassen
Picha: Anjum Naveed/AP/dpa/picture alliance

Kukamatwa kwa Khan katika maeneo ya mahakama wakati akijiandaa kuwasilisha ombi la dhamana, kulielezwa kuwa kinyume cha sheria siku ya Alhamisi na Mahakama ya Juu.

Mahakama hiyo iliendelea kumuweka rumande Khan hadi Ijumaa, ambako alipatiwa dhamana ya wiki mbili.

Mahakama Kuu ya Islamabad pia imeamuru Khan asikamatwe kabla ya Jumatatu katika kesi yoyote ile.

Wakati huo huo, watu wapatao 13 wakiwemo wanajeshi wameuawa katika shambulizi lililotokea kwenye kituo cha usalama kusini magharibi mwa Pakistan.