1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri mkuu wa zamani Ufaransa ajitosa kuwania urais 2027

4 Septemba 2024

Aliyewahi kuwa waziri mkuu nchini Ufaransa Edouard Phillipe ametangaza kugombea urais mwaka 2027 hatua ambayo inazidi kuitikisa hali ya kisiasa nchini humo baada ya uchaguzi wa bunge.

https://p.dw.com/p/4kHM7
 Ufaransa | Edouard Phillipe
Waziri mkuu wa zamani nchini Ufaransa Edouard PhillipePicha: Castel Franck/ABACA/IMAGO

Bado Rais Emmanuel Macron anahangaika kutafuta waziri mkuu mpya tangu aliposhindwa kukiimarisha chama chake kupitia uchaguzi wa bunge uliofanyika mwezi Julai.

Kushindwa kwa chama chake kumesababisha mkwamo wa kisiasa huku muungano wa mrengo wa kushoto ukihodhi idadi kubwa ya viti katika bunge ambalo halina mshindi wa moja kwa moja.

Soma pia:Macron aongeza juhudi za kuvunja mkwamo wa kisiasa

Wakati mazungumzo ya kuumaliza mkwamo wa kisiasa yakiendelea waziri mkuu wa zamani Eduardo Phillipe amethibitisha atagombea urais kurithi nafasi ya Macron, ambaye hawezi kugombea tena mwaka 2027 muhula wake wa pili utakapofikia mwisho.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW