1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUholanzi

Waziri mkuu wa Uholanzi Mark Rutte amejiuzulu

8 Julai 2023

Serikali ya mseto ya Waziri Mkuu wa Uholanzi Mark Rutte imevunjika kutokana na tofauti "zisizoweza kutatuliwa" kuhusu jinsi ya kukabiliana na uhamiaji, huku uchaguzi ukitarajiwa mwezi Novemba.

https://p.dw.com/p/4Tc99
Serbien | Premierminister Mark Rutte
Picha: Amir Hamzagic/AA/picture alliance

Kiongozi huyo wa muda mrefu zaidi wa Uholanzi na mmoja wa wanasiasa wenye uzoefu zaidi barani Ulaya, amesema baada ya siku kadhaa za  mazungumzo kuhusu mgogoro huo kati ya vyama vinne, wameshindwa kufikia makubaliano.

Mpasuko huo unajiri kufuatia mpango ya Rutte wa kuweka vizuizi vya kuziunganisha tena familia za wanaotafuta hifadhi.

Soma pia: Merkel na Rutte wajadili mageuzi ya Ulaya

Baada ya waziri mkuu huyo kujiuzulu, tume ya uchaguzi ya Uholanzi imesema uchaguzi wa mapema zaidi unaweza kuandaliwa katikati ya Novemba, huku Rutte akisema ataingoza serikali ya muda hadi wakati huo.