Waziri mkuu wa Somalia aapishwa
24 Novemba 2007Matangazo
Bunge nchini Somalia limemuapisha waziri mkuu mpya, Nur Hassan Hussein hii leo, likiwa na matumaini ya kuiimarisha serikali ya mpito ambayo imedhoofishwa na mkwamo wa kisiasa na vita dhidi ya wanamagambo.
Nur Hassan aliyeteuliwa mapema juma hili ameapishwa baada ya wabunge 211 kati ya wabunge 212 kumuidhinisha huko mjini Baidoa, makao makuu ya serikali ya mpito ya Somalia.
Hussein ameahidi ataiongoza Somalia kwa uaminifu na atafanya kila awezalo kuiimarisha.