1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaJapan

Tokyo, Waziri Mkuu wa Japan aahidi kufanya mageuzi

28 Oktoba 2024

Waziri Mkuu wa Japan Shigeru Ishiba ameahidi kufanya kile alichokiita mageuzi ya msingi baada ya chama chake na mshirika wake mdogo serikali kupata matokeo mabaya kabisa ya uchaguzi wa mapema wa bunge.

https://p.dw.com/p/4mIn7
Waziri Mkuu wa Japan Shigeru Ishiba
Waziri Mkuu wa Japan na kiongozi wa chama tawala cha LDP Shigeru Ishiba akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari baada ya uchaguzi wa bunge, Oktoba 28, 2024Picha: Kim Kyung-Hoon/REUTERS

Chama chake cha LDP pamoja na mshirika wake Komeito vimepata kwa pamoja jumla ya vitu 215 kati ya viti 465 vya bunge, yakiwa ni matokeo mabaya kabisa kwa muungano huo tangu mwaka 2009.

Waziri Mkuu Ishiba amesema leo Jumatatu kwamba ataanzisha mageuzi ya msingi kuhusiana na suala la fedha na siasa, huku akisisitiza atabakia madarakani na hatoruhusu ombwe la kisiasa.

Kwa mujibu wa Ishiba, kushindwa kwa muungano tawala kumesababisha na ukosefu wa imani na hasira za wapiga kura kutokana na kashfa matumizi mabaya ya fedha iliyokikumba chama chake.