Waziri Mkuu wa Japan aahidi msaada zaidi kwa Ukraine
22 Machi 2023Zelensky alimtaja Kishida kuwa mtetezi shupavu wa taratibu za kimataifa na rafiki wa muda mrefu wa Ukraine.
Naibu Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Ukraine Emine Dzheppar aliisifu ziara hiyo ya kihistoria akisema ni ishara ya ushirikiano wenye nguvu kati ya nchi hizo mbili.
Kishida aliiahidi Ukraine msaada wa kifedha pamoja na wa kiutu na matibabu. Waziri Mkuu huyo wa Japan alitarajiwa kurejea Tokyo baada ya ziara yake ya India, lakini akaibadili mipango yake na kuzuru Ukraine.
Wakati wa ziara yake, Kishida alitembelea Bucha, mji wa mdogo karibu na Kyiv ambako maafisa wa eneo hilo wanasema mamia ya miili ya raia ilipatikana.
Japan imejiunga na washirika wa Magharibi katika kuiwekea vikwazo Urusi kwa uvamizi wake wa Ukraine.
Kishida alikuwa ndiye kiongezi pekee wa kundi la nchi tajiri ulimwenguni - G7 ambaye hakuwa amezuru Ukraine tangu Urusi ilipoanza uvamizi kamili nchini humo Februari 2022.