1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaJapan

Waziri Mkuu wa Japan asema anazingatia ziara ya Ukraine

25 Januari 2023

Waziri Mkuu wa Japan Fumio Kishida amesema anafikiria kuitembelea Ukraine baada ya kupata mualiko kutoka kwa rais wa taifa hilo Volodymyr Zelensky.

https://p.dw.com/p/4MfZq
Japan | Parlament | Premierminister Fumio Kishida
Picha: YUICHI YAMAZAKI/AFP/Getty Images

Waziri Mkuu wa Japan Fumio Kishida, ambaye nchi yake ndio mwenyeji wa mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Kigeni wa kundi la mataifa saba tajiri duniani - G7, amesema anafikiria kuitembelea Ukraine baada ya kupata mualiko kutoka kwa rais wa taifa hilo Volodymyr Zelensky.

Kishida ameliambia bunge la nchi hiyo kwamba hadi sasa hajaamua kuhusu ziara hiyo lakini uamuzi wake utafuatiwa na masharti kadhaa bila ya kufafanua zaidi. Japan imekuwa ikifanya kazi na washirika wake wa mataifa ya G7 kuiwekea vikwazo Urusi kufuatia uvamizi wake Ukraine pamoja na kuiunga mkono nchi hiyo kwa kuwapa hifadhi raia wake wanaokimbia mapigano.

Iwapo ziara yake hiyo itafanikiwa kufanyika itakuwa ziara ya kwanza ya afisa wa ngazi ya juu wa Japan kufika Ukraine wakati huu ambako mapigano yanaendelea. Japan itakuwa mwenyeji wa mkutano wa G7 utakaofanyika Hiroshima mwezi Mei na mgogoro wa Ukraine unatarajiwa kuwa katika ajenda ya mambo makuu yatakayozungumziwa.