SiasaJapan
Waziri mkuu wa Japan aanza ziara ya ghafla Ukraine
21 Machi 2023Matangazo
Ziara hizo za kilele zinakuja katika wakati ambapo mahasimu hao wa muda mrefu wako katika mapambano ya kuoneshana nguvu kidiplomasia. Waziri mkuu Kishida wa Japan atakutana na rais Volodymyr Zelensky mjini Kiev.
Kwa mujibu wa wizara ya mambo ya nje ya Japan, kiongozi huyo ataonesha mshikamano na uungaji mkono kwa Ukraine, na kuupongeza ushujaa na subira ya waukraine waliosimama kidete kuitetea nchi yao chini ya uongozi wa rais Zelensky.
Katika mazungumzo yake anatarajiwa pia kuipinga Urusi na uvamizi wake nchini Ukraine.