Waziri Mkuu wa Italia kujiuzulu
Matangazo
Akilihutubia taifa kupitia televisheni baada ya matokeo ya awali kutangazwa, Renzi amesema majukumu ya serikali yake yamemalizika leo. Matokeo hayo yanaonyesha kambi yake ya kura ya 'Ndiyo' imeshindwa katika uchaguzi huo kwa kupata kati ya asilimia 42 na 46. Kambi ya 'Hapana' imepata kati ya asilimia 54 na 58 ya kura. Renzi amesema leo mchana ataitisha kikao na baraza lake la mawaziri na kisha atawasilisha barua yake ya kujiuzulu kwa Rais Sergio Mattarella.