SiasaItaly
Waziri Mkuu wa Italia kuitembelea Ukraine
21 Februari 2023Matangazo
Meloni anaizuru Ukraine baada ya kuitembelea Poland hapo jana ambako alitoa ahadi kwamba Italia itaendelea kuisaidia serikali mjini Kyiv ikiwa ni pamoja na msaada ziada wa kifedha, kijeshi na ule wa kiutu.
Mwanasiasa huyo wa mrengo wa kulia aliyechukua hatamu za uongozi nchini Italia Oktoba iliyopita, alizungumzia mara kadhaa dhamira yake ya kuitembelea Ukraine kuonesha mshikamano na nchi hiyo kufuatia uvamizi wa Urusi.
Italia iliyo mwanachama wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO tayari imeipatia Ukraine msaada wa fedha na silaha na mapema mwezi huu iliridhia kutuma mfuko wa kujilinda na makombora ulioundwa kwa pamoja kati ya nchi hiyo na Ufaransa.