Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, serikali ya Jean-Michel Sama Lukonde sasa ipo tayari kufanya kazi baada ya kuapishwa bungeni jana Jumatatu. Serikali hiyo mpya illiapishwa baada ya mpango wake kuidhinishwa na wabunge 410 kati ya 412 waliokuwepo wakati wa uwasilishaji wa mpango huo wenye nguzo 15 zinazolenga sekta nne. Sikiliza ripoti ya, Jean Noel Ba-Mweze anaripoti toka Kinshasa