1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaNew Zealand

Waziri Mkuu wa China aanza ziara nchini New Zealand

13 Juni 2024

Waziri Mkuu wa China, Li Qiang amewasili nchini New Zealand kuanza ziara ya nadra kwenye taifa hilo ambalo ni mshirika wake wa karibu miongoni mwa mataifa ya kidemokrasia yanayoegemea maadili ya nchi za magharibi.

https://p.dw.com/p/4gyW6
Waziri Mkuu wa China, Li Qiang
Waziri Mkuu wa China, Li Qiang.Picha: Florence Lo/REUTERS

Alilakiwa kwa shamra shamra kwenye uwanja wa ndege wa mji mkuu Wellington na anatarajiwa baadae leo kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa New Zealand Christopher Luxon na kisha kushirika dhifa ya heshima ya chakula cha jioni.

Ajenda ya juu ya ziara ya Qiang ni masuala ya biashara katika wakati Beijing inalenga kutuliza wasiwasi wa mataifa ya kanda ya kusini mwa bahari ya Pasifiki kutokana na kutanuka kwa ushawishi na nguvu za kijeshi za China.

Li ambaye ni kiongozi wa pili kwa nguvu za madaraka nchini China atazitembelea pia Australia na Malaysia katika safari yake hiyo ya nchi za nje ya siku sita.