1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri Mkuu Netanyahu anaaza ziara barani Ulaya

4 Juni 2018

Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu,anaanza ziara katika nchi za Ulaya. Kituo cha kwanza cha ziara yake ni Ujerumani  ambako anakuja katika nchi ambayo ina mafungamano na Israel.

https://p.dw.com/p/2ytgO
Berlin Deutsch-Israelische Regierungskonsultationen Netanjahu Merkel
Picha: Getty Images/AFP/O. Andersen

Uhusiano wa nchi zote mbili unajengeka  kutokana na maovu ya kihistoria-mauaji ya wayahudi milioni sita yaliofanywa na utawala wa Wanazi wa Ujerumani. Tangu mwaka 1965, uhusiano umekuwa ukiboreka na huo ndiyo mwaka ambao Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani lilianza uhusiano wa kibalozi na Israel. Upatanishi ulitokana zaidi  na David Ben Gurion ( 1886-1973). Licha ya mauaji ya kimbari Waziri mkuu huyo wa kwanza wa Israel aliiona nchi hii kuwa ni Ujerumani nyengine. Ben Gurion na Kansela wa kwanza wa Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani Konrad Adenauer walikutana mara mbili tu- 1960 na 1966-  na pamoja na hao viongozi wote wawili walionekana kuwa kama marafiki wa mbali.

Msimamo wa Ujerumani kwa Israel

Benjamin Netanjahu Ministerpräsident Israel
Waziri Mkuu wa Isreal Benjamin NetanyahuPicha: Getty Images/AFP/S. Scheiner

Leo uhusiano wa nchi hizi ni  wa ushirikiano. Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Ujerumani Heiko Maas ameueleza uhusiano wa nchi hizi mbili kabla ya ziara yake ya Israel  kwa kusema "Ninaamini kwamba takriban sote tunakubaliana kuna tafauti njiani lakini daima Ujerumani itakuwa upande wa Israel katika masuala yote haya.”

Kumbukumbu ya mauaji makubwa ya Wayahudi ni muhimu  anasema  mwaandishi habari Mjerumani – Muisraili Michael Wolffsohn. Anaipinga ile hoja kwamba  mauaji ya kimbari Holocaust  ndiyo yaliosababisha kuundwa dola ya Israel: Anasema, " Hilo lazima tulisahihishe. Israel ingekuwepo hata bila ya mauaji ya kimbari na  wayahudi milioni sita wangeweza kunusurika.Tofauti za Isra

Tofauti za Israel na Ujerumani

Ujerumani na Israel zinakubaliana mengi. Lakini pia kuna  masuala yenye utata hasa panapohusiana na  mgogoro wa zaidi ya miaka mia moja kati ya Waisraili na Wapalestina. Zaidi ya hayo baadhi ya vyombo vya habari vingali vikizungumzia uhalali wa kuwepo Israel.Sambamba na hayo ni  suala zima la usalama wa dola la Israel.

Waisraili kwa wakati huu wanaangalia kwa hali ya kukerwa, kuwepo kwa hisia za chuki dhidi ya Wayahudi nchini Ujerumani na Ulaya, iwe ni kutoka mrengo wa kushoto, kulia au hata itikali kali za kiislamu. Kwa upande wa Ujerumani Kunakosekana hali ya kuashiria  amani kati ya Israel na Wapalestina.Pamoja na yote lakini mshikamano na Israel ni sehemu ya msimamo wa Ujerumani. Katika hotuba yake ya kihistoria mbele ya bunge la Israel-Knesset 2008, Kansela alitoa kauli ya msisimko alipotamka maneno haya " Kila serikali ya Shirikisho na  kila Kansela wa Shirikisho aliyenitangulia alijizatiti katika jukumu  maalum la kihistoria kwa ajili ya usalama  wa Israel."

Kwa muda mrefu ,Ujerumani ni mshirika  wa pili muhimu wa kibiashara wa Israel baada ya Marekani na  huipatia nyambizi dola la Israel. Kuna miradi kadhaa ya pamoja ya shughuli za  utafiti .

Leo hii Ujerumani na Israel zinakubaliana  katika mambo mengi.Lakini pia kuna  masuala  kama ujenzi wa makaazi ya walowezi wakiyahudi. Wengi wa Waisraili wanawashutumu Wajerumani na  wengineo barani Ulaya kwa kushindwa kukabiliana  ipasavyo na nchi zenye uadui na Israel. Bila shaka uhusiano wa kisiasa haukosi mivutano. Mbali na Ujerumani Netanyahu atazizuru pia Ufaransa na Uingereza.

Mwandishi: Mohammed Abdul-Rahman/ Knipp,Kersten (DW)
Mhariri:Josephat Charo