Waziri mkuu mpya wa Somalia atoa wito wa mazungumzo
2 Desemba 2007Matangazo
Mogadishu:
Waziri mkuu wa Somalia leo ametoa wito wa mazungumzo na wapinzani kumaliza uasi wa wanaharakati wa Kiislamu katika mapambano ambayo yanasemekana yamewauwa karibu raia 6,000 tangu yalipoanza mwaka jana. Katika baadhi ya matamhi yake ya kwanza hadharani waziri mkuu huyo mpya wa Somalia Nur Hassan Hussein alisema yuko tayari kuzungumza na muungano wa makundi ya upinzani wenye makao yake makuu nchini Eritrea.
Hussein aliteuliwa kuiongoza serikali ya mpito mwishoni mwa mwezi uliopita kuchukua nafasi ya Ali Mohammed Gedi aliyefutwa kazi baada ya mvutano na Rais Abdulahi Yussuf Ahmed. Somalia imo katika vurugu na mapigano ya wenyewe kwa wenyewe tangu ulipoangushwa utawala wa Muhammad Siad Barre 1991.