Waziri Mkuu mpya wa Haiti aahidi kutafuta umoja wa kitaifa
30 Mei 2024Matangazo
Kwenye ujumbe huo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa X, Conille ayeliwahi hapo kabla pia kuwa waziri mkuu wa Haiti kati ya Oktoba 2011 hadi Mei 2012 amesema ananuwia kufanya kazi pamoja na makundi yote nchini humo kufanikisha hatma njema kwa watoto wa taifa hilo.
Soma pia:Biden na Ruto kukutana mjini Washington
Ametumia ujumbe huo pia kuwashukuru makundi ya kiraia, vyama vya siasa na raia wa Haiti waishio nje ya nchi kwa kulipendekeza jina lake ili ateuliwe kuchukua nafasi ya waziri mkuu.
Kazi kubwa inayomkabili ni kupambana na uhalifu wa magenge ambayo yanadhibiti asilimia 80 ya mji mkuu, Port au Prince na kurejesha utulivu na amani nchini humo.