Waziri Mkuu mpya ameapishwa Somalia
25 Novemba 2007Matangazo
Bunge nchini Somalia limemuapisha Waziri Mkuu mpya,Nur Hassan Hussein,anaetazamiwa kuimarisha serikali ya mpito nchini humo.Hussein aliyeteuliwa mapema juma hili,ameapishwa baada ya kuidhinishwa na wabunge 211 kutoka 212 mjini Baidoa,makao makuu ya serikali ya mpito.Hussein ameahidi kuiongoza Somalia kwa uaminifu na atafanya kila awezalo kuimarisha nchi.