Waziri Mkuu mpya achaguliwa Somalia
22 Novemba 2007Matangazo
Rais Abdullahi Yusuf wa Somalia amemteua Nur Hassan Hussein kama waziri mkuu mpya,ikiwa ni majuma matatu baada ya mtangulizi wake Ali Mohamed Gedi kujiuzulu kufuatia mivutano ya kisiasa.Rais Yusuf amesema,anatumaini kuwa Hussein ataunda serikali itakayoweza kufanya kazi na kuiokoa nchi kutoka janga la hivi sasa.
Kwa upande mwingine,shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia wakimbizi(UNHCR) linatathimini kuwa kiasi ya watu 600,000 wameukimbia mji mkuu wa Somalia,Mogadishu kujiepusha na mapigano. Vikosi vya Ethiopia na vya serikali ya Somalia vinapambana na wanamgambo wenye itikadi kali za kiislamu.