Waziri Mkuu ajaye wa Japan ataja vipaumbele vyake
27 Septemba 2024Waziri Mkuu ajaye wa Japan Shigeru Ishiba leo ameweka wazi malengo yake ya kisera anayosema yatalibadili taifa hilo mshirika wa Marekani, saa chache baada ya kupata ushindi wa kukiongoza chama tawala cha Liberal Democratic.
Ishiba mwenye umri wa miaka 67 na waziri wa zamani wa ulinzi ameahidi kurekebisha haiba ya chama chake kufuatia mfululizo wa kashfa zilizokiandama pamoja na kutimiza ahadi za kuboresha maisha ya umma wa nchi hiyo.
Soma: Japan yamchagua waziri mkuu mpya Shigeru Ishiba
Amesema miongoni mwa ajenda yake ya kipaumblee na kurejesha utulivu kwenye kanda ya Pasifiki ambayo imetumbukia kwenye mivutano na uhasama hasa kutokana na kutanuka kwa ushawishi na kiuchumi na nguvu za kijeshi za China.
Ishiba atachukua mikoba ya uongozi wa taifa hilo mwanzoni mwa Oktoba kumrithi Fumio Kishida aliyetangaza mwezi Agosti kuachia uongozi wa chama tawala na kupiteza wadhifa wa uwaziri mkuu.