1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri Jung atembelea wanamaji wa Ujerumani nchini Lebanon

29 Februari 2008
https://p.dw.com/p/DFfZ

BEIRUT:

Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani Franz Josef Jung amewasili nchini Lebanon kutembelea kikosi cha wanamaji cha Ujerumani.Kikosi hicho cha Ujerumani kilikuwa kikiongoza majeshi ya Umoja wa Mataifa UNIFIL kwenye pwani ya Lebanon tangu mwaka moja na nusu.Sasa kinapokewa na Italia kuongoza vikosi vya wanamaji vya Ulaya ikiwa ni pamoja na manowari za Ufaransa,Hispania na Ureno.Kikosi cha wanamaji wa Ujerumani wapatao 500 kitabakia pamoja na manowari nne badala ya manowari saba.

Wanamaji hao watakuwa sehemu ya kikosi cha UNIFIL kilichoundwa kuzuia usafirishaji haramu wa silaha kwa kundi la Hezbollah baada ya kumalizika vita vya mwaka 2006 kati ya Israel na Lebanon.