Waziri Gates ajaribu kupunguza mvutano wa NATO
8 Februari 2008Matangazo
VILNIUS:
Waziri wa Ulinzi wa Marekani Robert Gates amejaribu kupunguza mvutano katika Jumuiya ya Kujihami ya Nchi za Magharibi-NATO kufuatia onyo la kutokea mgawanyiko katika harakati za washirika wa jumuiya hiyo.Gates amesema anazielewa nchi shirika kama Ujerumani isiyotaka kupeleka kikosi cha mapigano kusini mwa Afghanistan.Amesema nchi isiyotaka kupeleka vikosi vingeweza kusaidia kwa kuchangia helikopta zaidi.Gates alikuwa akizungumza kwenye mkutano wa mawaziri wa ulinzi wa Nato unaomalizika leo hii katika mji mkuu wa Lithuania Vilnius.