1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jeshi la Israel ladaiwa kuwajeruhi Wapalestina wawili

10 Aprili 2023

Wizara ya Afya ya Palestina imesema vikosi vya Israel vimewafyatulia risasi na kuwajeruhi Wapalestina wawili na kumuua mmoja wakati wa msako wao katika kambi ya wakimbizi ya Jeriko.

https://p.dw.com/p/4Ps6N
Israel Westjordanland Attacke Schießerei Attentat Polizei
Picha: Mohammed Torokman/REUTERS

Wizara ya Afya ya Palestina imesema vikosi vya Israel vimewafyatulia risasi na kuwajeruhi Wapalestina wawili na kumuua mmoja wakati wa msako wao katika kambi ya wakimbizi ya Jeriko, iliyopo kwenye eneo lenye kukaliwa kimabavu la Ukingo wa Magharibi.

Pasipo maelezeo ya kina, jeshi la Israel limesema vikosi vyake vilikuwa vinatekeleza majukumu yake katika kambi ya Aqabat, iliyo karibu na Jeriko.

Wizara ya afya ya Palestina imesema watu hao walishambuliwa kwa risasi za moto walizopigwa katika masafa ya karibu na kwamba majeruhi wamepelekwa kwenye hospitali moja ya Jeriko.