Wawekezaji wapuuza changamoto za Afrika
14 Novemba 2014Lakini kwa wawekezaji wengi wapya, hayo yote hayawazuii kuendelea na mipango yao barani humo. Hata wakati kukiwa na matatizo mengine kuhusu kupungua bei za vyakula na uwezekano wa kupanda viwango vya riba nchini Marekani, wawekezaji katika eneo la chini ya jangwa la Sahara wanasisitiza kuwa bado wanaona uwezo mkubwa wa ukuaji, unaotokana na kuimarika biashara ya kikanda, uwekezaji unaokua pamoja na idadi kubwa ya watu wa tabaka la kati.
Ukuaji usiotetereka tunaoshuhudia duniani unatoka barani Afrika amesema Asha Meghat msimamizi wa hazina ya kimataifa ya mfuko wa usawa yenye thamani ya dola milioni 380, Meghat amesema na hali hiyo ya Ukuaji wa kiuchumi barani afrika huenda ikawa hivyo kwa miaka Kumi ijayo.
Kujitokeza kwa masoko yanayochipukia katika miaka hii yamekuwa na woga wa kushuka kwa uchumi wa China na hali ya juu ya uchumi wa Marekani.
Vitisho vya usalama vinavyosababishwa na Boko Haram na Al Shabaab, mgogoro wa Kisiasa nchini Burkina Faso au kadhia ya mripuko wa Ebola ambao umesababisha vifo vya maelfu ya watu katika eneo la Afrika Magharibi, vinawakumbusha wawekezaji kuwa wana kazi ngumu ya kufanya katika miongo kadhaa barani humo.
Kushuka kwa uchumi wa China pia kumeathiri uchumi wa Afrika bara ambalo kwa bahati limekuwa likijitahidi sana katika sekta ya madini na utafutaji wa mafuta ambao umeongeza moja kwa moja wawekezaji wa Kichina.
Lakini mwekezaji kama Jonathan Stichbury ambaye ni mkurugenzi mtendaji wa Pine Bridge ya Afrika Mashariki ambaye ana dola bilioni 2.2 chini ya usimamaizi wa kikanda, ukiiondoa Afrika Kusini, anasema ukuaji katika nchi za Afrika katika ukanda wa jangwa la sahara ni mdogo sana kujitegemea kutokana na bei za bidhaa na kwa kiasi kikubwa unaendeshwa na maendeleo yatokanayo na ardhi.
Alisema Nchi hizi zinafurahia kipindi cha ukuaji ambao nadhani karibu utasitishwa,akitoa sababu kama kuanguka kwa vikwazo vya kibiashara,kuondoa kwa udhibiti wa sarafu katika
nchi nyingi na kuibuka kwa tabaka la kati.
Kwa mfano idadi ya kaya za tabaka la kati ni 11 kwa mataifa yenye uchumi wa juu kwa nchi za Afrika zilizo katika ukanda wa jangwa la sahara imepungua kutoka asilimia 230 kwa miaka 14 iliyopita hadi milioni 15 na hii ni kwa mujibu wa ripoti ya Standard Bank; na idadi hiyo inatarajiwa kupanda kwa milioni 40 ifikapo mwaka 2030.
Shirika la fedha duniani limesema uchumi wa nchi zilizo katika jangwa la sahara utakuwa kwa asilima 5 mwaka huu, na utapanda kwa silimia 5.8 katika mwaka wa 2015. Nigeria ni nchi yenye uchumi mkubwa Afika na itakuwa kwa asilimia 7.3 mwaka ujao wakati Kenya ikiwa katika mstari wa kuongeza asilimia 6.2 kulinganisha na utabiri wa kimatifa kwa uchumi unaokuwa kwa asilimia 3.9.
Taarifa kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika inaonesha kweli kuwa ni robo tu ya nchi za Afrika zinazalisha mafuta, na baadhi ya nchi katika bara hilo ni masikini kama vile Liberia na Sierra Leone zinazotumia asilimia 15 ya mapato yao kuagiza mafuta, AfDB inasema kwa wao kuanguka kwa asilimia 25 ya mafuta mwaka huu itakuwa mafanikio
Mwandishi: Nyamiti Kayora
Mhariri:Yusuf Saumu