1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wavuvi wauguwa ugonjwa wa ajabu Guinea

21 Aprili 2023

Zaidi ya wavuvi 50 nchini Guinea wamelazwa hospitali kwa ugonjwa wa ngozi ambao haujatambulika, siku moja baada ya mamlaka nchini humo kuanzisha uchunguzi wa tukio hilo.

https://p.dw.com/p/4QPtw
Guinea l Übergangspräsident Mamady Doumbouya
Picha: uncredited/AP/picture alliance

Picha zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii zimeonyesha nyuso za wavuvi, midomo na mikono ikiwa na vipele na vidonda.

Msemaji wa serikali, Ousmane Diallo, amesema serikali tayari imeunda kamati yenye wawakilishi kutoka wizara za mazingira, uvuvi, afya, uchukuzi na madini.

Soma zaidi:Burkina Faso, Guinea na Mali wapanga ushirikiano 

Aidha kamati ya wanasayansi imechukua sampuli za maji ya bahari katika maeneo yanayoshukiwa, na sampuli hizo zinachunguzwa katika maabara za ndani na nje ya nchi.

Uchunguzi uliofanywa katika bidhaa za uvuvi zilitolewa na wavuvi hao walioathirika zinaonyesha kuwa ni salama kwa kuliwa.