1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroSudan

Wanamgambo wawaua watu 18 nchini Mali

27 Mei 2024

Watu wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wa itikadi kali wamewauwa raia 18 katikati mwa Mali.

https://p.dw.com/p/4gKME
Mali | Kanali Assimi Goita
Kanali Assimi Goita, kiongozi wa muda wa Mali. Taifa hilo linakabiliwa na mashambulizi ambayo hivi karibuni yamewaua watu karibu 18 Picha: OUSMANE MAKAVELI/AFP/Getty Images

Haya ni kulingana na vyanzo kadhaa vilivyozungumza na shirika la habari la Ufaransa AFP. Raia watatu wa kijiji hicho cha Diallassagou wamesema kuwa idadi ya waliojeruhiwa ni watu 21.

Afisa mmoja ameliambia shirika hilo la AFP kuwa wahanga hao wa mashambulizi hayo wote walikuwa wamekimbia mapigano na walikuwa wamekita kambi katika kijiji hicho.

Mnamo Juni mwaka 2022, zaidi ya raia 130 waliuwawa katika kijiji kimoja, katika mojawapo ya mashambulizi mabaya zaidi kuwahi kushuhudiwa nchini Mali katika miaka ya hivi karibuni.

Serikali ya Mali ilikinyoshea kidole cha lawama kundi la Katiba Macina lililo na mafungamano la Al-Qaeda kwa shambulizi hilo.