1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSenegal

Watu wawili wauwawa wakati wa maandamano, Senegal

1 Agosti 2023

Wizara ya usalama wa ndani nchini Senegal imesema watu wawili wameuwawa wakati wa maandamano kusini mwa nchi hiyo, kufuatia kufikishwa mahakamani na kushikiliwa kwa kiongozi wa upinzani, Ousmane Sonko.

https://p.dw.com/p/4UdKC
Wafuasi wa kiongozi wa upinzani nchini Sengal Ousmane Sonko wafanya maandamano
Wafuasi wa kiongozi wa upinzani nchini Sengal Ousmane Sonko wafanya maandamano Picha: NGOUDA DIONE/REUTERS

Wizara hiyo ya mambo ya ndani imesema maandamano hayo yalizuka mchana wa jana katika mji wa Zuguinchor, ambapo miili miwili ya wanaume iligunduliwa. Taarifa ya wizara hiyo kwa vyombo vya habari haikutoa undani zaidi wa vifo hivyo katika mji huo ambao Sonko ndiye meya.

Chama cha PASTEF kuvunjwa

Chini ya masaa mawili baada ya Sonko kufikishwa mahakamani, wizara hiyo ya usalama wa ndani ilitangaza kwamba chama chake cha PASTEF kitavunjwa kwa kuwa mara kwa mara kimekuwa kikitoa wito wa mapinduzi, hatua iliyopelekea uharibifu wa mali na mauaji. Sonko anakabiliwa na kesi kadhaa ambazo mwenyewe anadai ni kwa ajili ya kumzuwia kushiriki uchaguzi wa rais Februari mwakani.